Connect with us

News

Zahoro Hanuna Achukua Fomu ya Kugombea Ubunge Bumbuli Kupitia CCM

Published

on

Na Mwandishi wetu, News Info Online

Zahoro Rashid Hanuna, leo Juni 28, 2025, amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Bumbuli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hanuna alipowasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga, alipokelewa na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mhe. M.S. Kaaya, ambaye alimkabidhi rasmi fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Hanuna si mgeni katika siasa za ndani ya CCM. Mwaka 2020 aligombea kura za maoni katika Jimbo la Kawe, na mwaka 2021 alijitokeza kuwania nafasi ya uspika wa Bunge kupitia chama hicho.

Hatua yake ya kuchukua fomu leo inaashiria mwendelezo wa safari yake ya kisiasa, akilenga kuwawakilisha wananchi wa Bumbuli bungeni kupitia tiketi ya CCM

Continue Reading
Click to comment
0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

News

Rais Mwinyi aizawadia Yanga Milioni 100

Published

on

Na Mwandishi wetu, News Info

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameizawadia Klabu ya Yanga SC shilingi milioni 100, kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa waliopata katika msimu wa mwaka 2024/2025.


Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 30 Juni 2025 alipokutana na viongozi pamoja na wachezaji wa Yanga waliofika Ikulu kwa ajili ya kumkabidhi makombe matano ya michuano mbalimbali waliyoyatwaa msimu huu.


Akizungumza nao, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana na klabu hiyo kongwe, akieleza kuwa yanajenga heshima na historia muhimu katika tasnia ya michezo nchini.


Aidha, ameishukuru Yanga kwa kuendelea kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya nchi kupitia kampeni ya Visit Zanzibar, huku akieleza kuwa hatua ya klabu hiyo kucheza baadhi ya michezo yake Zanzibar kunachangia kukuza uchumi na sekta ya utalii kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wageni na wananchi kunufaika na fursa mbalimbali.

Continue Reading

News

Stan Bakora achukuwa fomu kugombea udiwani Morogoro Mjini

Published

on

Na Mwandishi wetu, News Info Online

Msanii Stanbakora amechukua Fomu ya kuomba ridhaa ya Kugombea Udiwani Morogoro Mjini Kata ya Kiwanja Cha Ndege kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika.
“Wana MOROGORO MJINI Kata Ya KIWANJA CHA NDEGE Nipo Tayar Kuwatumikia”

SatMediaUpdates

Continue Reading

News

FCC YATOA SEMINA YA MASUALA YA UHIBITI BANDIA KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE

Published

on

Na Mwandishi wetu, Newsinfo Online

Tume ya Ushindani (FCC) imeendesha semina maalum ya Uhamasishaji wa masuala ya ushindani, kumlinda mlaji na udhibiti wa Bidhaa bandia kwa wanawake wajasiriamali Mkoa wa Dar es Salaam, kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo Sheria zinazosimamia masuala ya Ushindani nchini.

Semina hiyo ya siku moja imefanyika June 13, 2025 katika Ofisi za FCC Jijini Dar es Salaa,  kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), ili kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) kuelewa zaidi sheria na kanuni za ushindani wa haki zitakazosaidia kufanya shughuli zao kwa weledi.

Akizungumza alipokuwa akifungua kikao hicho, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bi. Khadija Ngasongwa, Mkurugenzi wa Tafiti, Muungano wa Makampuni na Uraghibishi Bi. Zaytun Kikula, amesema mafunzo hayo yana mchango mkubwa katika kuimarisha mazingira ya Biashara nchini.

“Jukwaa hili linaturuhusu kushirikiana moja kwa moja na wamiliki wa biashara, kuwaelimisha juu ya sheria za ushindani, na kuhakikisha wanajenga biashara imara na endelevu,” alisema.

Aidha, Bi. Kikula amesema anaamini kuwa wafanyabiashara wanawake wana nafasi kubwa katika maendeleo ya kiuchumi, ustawi wa familia na ukuaji wa jamii, nakwamba utowawezesha kuna athari ya moja kwa moja kwa jamii.

Amesisitiza kuwa kulinda biashara dhidi ya ushindani usio wa haki, pamoja na kuhakikisha wateja wanapokea bidhaa na huduma bora, inasalia kuwa sehemu ya msingi ya mamlaka ya FCC.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa TWCC Bi. Mwalongo Kambewe amewataka washiriki kutumia mafunzo waliyoyapata kuimarisha shuguli zao, huku akibainisha kuwa maarifa huleta mabadiliko

Kila unapojifunza unakua” Bi. Kambewe amesema na kuongeza kuwa “Ninaamini wanawake hawa wataona mabadiliko sio tu katika biashara zao bali hata katika familia na jamii zao. amesema.

Naye Kaimu Meneja wa Makubaliano ya Washindani wa FCC, Bw. David Mawi, akizungumza alipokuwa akitoa wasilisho katika semina hiyo, amesisitiza kuwa soko huria haliwezi kuendelea bila kuwepo udhibiti.

“Soko huria haliwezi kuendelea bila mdhibiti, Tunahitaji kulinda biashara na watumiaji dhidi ya mazoea yasiyo ya haki ambayo mara nyingi yanalenga washiriki wadogo au wapya kwenye soko.” Amesema Bw. Mawi

Ameongeza kuwa kutumia vibaya utawala wa soko, unaofafanuliwa kama kudhibiti zaidi ya asilimia 40 ya hisa ya soko kwa muda endelevu, ni ukiukaji wa sheria na hatari ya kuwadhuru washindani na watumiaji.

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za FCC katika kuhakikisha wajasiriamali wanawake wa Kitanzania wanapata maarifa na kujengewa uelewa ili kufanikiwa katika soko la ushindani, ndani na nje ya nchi.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2025 Newsinfo.