News

Makonda Dkt. Samia ameonesha uwezo mkubwa wa kulinusuru taifa

Published

on

Na Mwandishi wetu, NewsInfo – Arusha

Mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paull Makonda, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha kwa vitendo uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto ambazo zingeweza kulipasua au kuligawa Taifa, lakini ameendelea kuliongoza kwa umoja na utulivu.

Akizungumza leo mbele ya wananchi wa Mkoa wa Arusha, Makonda alisema Dkt. Samia ameonesha uongozi imara unaofanana na misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ya watu kuishi kwa amani bila kujali kabila wala dini.

Amefafanua kuwa, moja ya sifa kubwa ya Dkt. Samia ni uwezo wake wa kulibeba taifa na kulifanya libaki moja, hususan katika vipindi vigumu kama wakati wa kifo cha Hayati Dkt. John Magufuli na kipindi cha janga la corona ambapo hata biashara nyingi ziliporomoka, lakini nchi iliendelea kuwa thabiti.

Makonda aliongeza kuwa mafanikio hayo yameendelea hadi sasa ambapo Tanzania inaingia kwenye kipindi cha uchaguzi huku uchumi ukiendelea kuimarika kwa kutumia fedha za ndani, jambo linaloonesha uongozi wa kidira na wa kizalendo wa Dkt. Samia.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

Trending

Exit mobile version