News

Mixx yazindua kampeni kubwa ya mwisho wa mwaka – “magift ya mixx pesa”

Published

on

Na Mwandishi wetu, Newsinfo Online

Mixx, imezindua kampeni kubwa ya mwisho wa mwaka – Magift ya Mixx Pesa- ikiwa ni shukrani kwa wateja wanaoendelea kuichagua Mixx, kila siku.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo inayoanza leo Disemba 1 na kutarajiwa kumalizika Disemba 4 mwaka huu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Bi. Angelica Pesha alisema ;

“Katika msimu huu wa sikukuu wenye mahitaji mengi, Mixx inakuja na zawadi nono kupitia kila muamala, ikiwemo milioni 1 kila siku, milioni 5 kila wiki, ushindi wa milioni 10 MixxMas, na mwaka mpya na Jackpot ya milioni 50 mwishoni mwa kampeni. Kampeni hii ni uthibitisho wa jinsi tunavyothamini uaminifu wa wateja wetu na dhamira ya kuendelea kubuni huduma rahisi, nafuu na zinazowawezesha katika malipo, akiba na mahitaji yote ya kifedha. Tunawaalika wateja wote kutumia huduma zetu za wakala, Mixx Super App au 15001# ili kupata nafasi ya kushinda na kuufunga mwaka kwa nguvu kupitia “Magift ya Mixx Pesa”

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara wa Mixx, Bw. James Sumari, alisema kuwa kwao kila Mtanzania ana nafasi ya kuanza safari yake ya kifedha kupitia huduma mbalimbali wanazotoa ikiwemo malipo, akiba, mikopo, bima na elimu ya fedha.

“Tunasema Mixx ni mshirika wako katika kila hatua ya safari ya kifedha kwa sababu dhamira yetu ni kuwaona Watanzania wakinufaika, wakikua na wakitimiza malengo yao ya maisha. Kupitia huduma zetu tunataka kila Mtanzania aweze kumudu mahitaji ya kila siku, kuanzisha au kukuza biashara, kujiandaa na majanga ya kifedha pamoja na kupata huduma za kifedha zilizo karibu, nafuu na zinazoaminika,” alisema Bw. Sumari.

Alisema Mixx inalenga kuwa sehemu ya mafanikio ya kila familia, kila kijana na kila mjasiriamali kwa kuwapatia huduma bora na teknolojia inayoeleweka na inayotumika kwa urahisi.

“Tunaamini leo tunachukua hatua nyingine muhimu hatua ya kushukuru, ya kuwezesha na ya kurudisha kwa wateja wetu. Hatua inayolenga kuimarisha nafasi yetu kama mwezeshaji wa kifedha nchini,” aliongeza.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

Trending

Exit mobile version