News
Nabii Mkuu Mhe. Dr. Geordavie ateuliwa kuwa balozi na mwakilishi wa UN-PAF wa Afrika Mashariki
Na Mwandishi wetu, Newsinfo Online
Nabii Mkuu Mheshimiwa Balozi Dr. GeorDavie K. Moses, Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Jijini Arusha, Ameteuliwa rasmi na Shirika la Mabalozi wa Amani la Umoja wa Mataifa UN-PAF kuwa Mwakilishi na Balozi wa Afrika Mashariki.
Mara baada ya uteuzi huu kufanyika jijini New York nchini Marekani tarehe 9.9.2025, Mwenyekiti wa Dunia wa UN-PAF, Mhe. Balozi Kingsley Ossai, ametuma barua za Utambulisho rasmi kwa Serikali ya Tanzania pamoja na United Nations chapter ya Tanzania na Ubalozi wa Marekani nchini, kwa dhumuni la kumtambulisha Mhe. Dr. GeorDavie katika wadhifa wake mpya.
Mhe. Dr. GeorDavie ambaye pia ni mlezi wa JMAT Taifa, amekuwa akifanya kazi za Ubalozi wa Amani na kugusa maisha ya watu mbalimbali hasa katika suala zima la kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kielimu na hivyo kumfanya aendelee kuwa nuru na alama ya amani, upendo na kung’ara kimataifa kutokea nchini Tanzania.
Tunaamini kama Balozi wa Amani Duniani, ataziwakilisha vema nchi za Afrika
