News

Rais Mwinyi aizawadia Yanga Milioni 100

Published

on

Na Mwandishi wetu, News Info

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameizawadia Klabu ya Yanga SC shilingi milioni 100, kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa waliopata katika msimu wa mwaka 2024/2025.


Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 30 Juni 2025 alipokutana na viongozi pamoja na wachezaji wa Yanga waliofika Ikulu kwa ajili ya kumkabidhi makombe matano ya michuano mbalimbali waliyoyatwaa msimu huu.


Akizungumza nao, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana na klabu hiyo kongwe, akieleza kuwa yanajenga heshima na historia muhimu katika tasnia ya michezo nchini.


Aidha, ameishukuru Yanga kwa kuendelea kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya nchi kupitia kampeni ya Visit Zanzibar, huku akieleza kuwa hatua ya klabu hiyo kucheza baadhi ya michezo yake Zanzibar kunachangia kukuza uchumi na sekta ya utalii kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wageni na wananchi kunufaika na fursa mbalimbali.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

Trending

Exit mobile version