Connect with us

News

Benki ya NMB yazindua Tawi maalum la NMB Tinde Mnadani

Published

on

Na Mwandishi wetu, Shinyanga

BENKI ya NMB imezindua tawi maalum la NMB Tinde Mnadani mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuzingatia dhamira yake ya muda mrefu ya kusambaza huduma za kifedha kwa jamii ambazo hazijafikiwa.

Uzinduzi huu umeambatana pamoja na uzinduzi wa matawi mengine maalum ya Itobo(Nzega, Tabora), Iboregero(Igunga, Tabora), Mkongeni(Mvomero, Morogoro) na Dosidosi(Kiteto, Manyara)

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo ,Afisa Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi ameeleza kuwa Benki hiyo inatambua nafasi muhimu ya minada ya mifugo katika uchumi wa vijijini na uwepo wake katika mnada wa Tinde unaashiria utoaji wa huduma za kifedha na dhamira ya Benki ya NMB kusogeza huduma hizi kwa kila mtanzania huku wakiziwezesha jamii ambazo kihistoria zimekuwa zikikabiliwa na vikwazo vya kufikiwa na huduma za kifedha.

Amesema eneo hilo la kimkakati la Tawi hili jipya maalum linalenga kuleta mapinduzi katika hali ya kifedha ya wafanyabiashara na wafugaji kwa kutoa huduma salama, rahisi na zenye ufanisi huku zikirahisisha na kuboresha shuguli zao kwa maslahi makubwa ya uchumi wa binafsi na wa mkoa wa Shinyanga kwa ujumla.

“Kwa kuanzisha tawi hili maalum ndani ya mnada wa Tinde, tunatatua changamoto za moja kwa moja za matumizi makubwa ya pesa taslimu kwa kituo hiki kitatoa huduma kamili, zikiwemo kuweka pesa na kutoa pesa, kufanya miamala mbalimbali, programu za elimu ya kifedha hususani zeney mlengo wa ufugaji na mkopo maalum iliyoundwa kuongeza tija ya mifugo na biashara kwa ujumla, ” Mponzi alisema.

Ameongeza kuwa, kabla ya hapo washiriki wa minada ya mifugo, wanunuzi na wafanyabiashara walilazimika kubeba pesa taslimu ili kuweza kufanya manunuzi au baada ya mauziano ya bidhaa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Mgeni Rasmi wa hafla hiyo, Dk Kalekwa Kasanga
“Uwekezaji huu wa Benki ya NMB utakuwa na faida kubwa kwa jamii yetu. Kwa kutoa njia salama na rahisi za kusimamia fedha, kupitia tawi hili maalum, uchumi wa Tinde utazidi kuimarika na watu wengi watanufaika zaidi na huduma hizi za kifedha na hivyo tutatengeza fursa za ajira na kuboresha hali ya jumla ya maisha kwa wakazi wetu.” Dk.Kasanga alisema.

“Kwa upatikanaji wa mikopo na fursa ya kuweka akiba, wafugaji wataweza kuwekeza katika mifugo iliyoboreshwa, lishe bora na mbinu za kisasa za ufugaji, na hivyo kusababisha tija kubwa na kuongeza kipato. Hii pia itachochea mahitaji ya bidhaa na huduma nyingine, na kujenga mzunguko mzuri wa ukuaji wa uchumi,” aliongeza.

Naye mfanyabiashara na mfugaji kutoka Tinde, Gerald Mwandu ameishukuru benki ya NMB kwa kujenga kituo hicho katika kata ya Tinde. Amewaomba wafugaji, wakulima na Wafanyabiashara kutumia huduma za benki mbalimbali za benki ya NMB

Continue Reading
Click to comment
0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

News

Wanawake 142 waanza mafunzo ya Female Future Programme Dar es Salaam

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Zaidi ya wanawake 142 wamepokelewa rasmi kushiriki toleo la 12 la programu ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake, Female Future Programme (FFP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ya kiutendaji yameandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI).

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran amesema programu hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwa zaidi ya wanawake 800 waliokwisha pata mafunzo kwa zaidi ya muongo mmoja, na sasa inaendeshwa katika nchi sita kwa ufadhili wa NHO, huku akiwahamasisha washiriki kushiriki kikamilifu safari ya miezi tisa ya mafunzo. Aidha, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI, Dkt. David Kalaba amesema jamii inahitaji wanawake viongozi wenye kujiamini na uwezo mkubwa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya haraka, akisisitiza umuhimu wa mtazamo wa kimataifa, kujifunza na kuendana na mabadiliko pamoja na uwezo wa kusimamia utofauti, kutatua migogoro na kutoa thamani kwa wateja.

Kwa upande wake, Meneja wa Upstream wa IFC, Bw. Sam Nganga aliyemwakilisha Meneja wa Nchi, Bi. Martine Valcin amesema taasisi hiyo inaendelea kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi katika ngazi za juu za uongozi ili kukuza ushirikishwaji, huku akiwahimiza washiriki kujisimamia na kutumia kikamilifu mafunzo hayo.

Katika hafla hiyo pia kulikuwa na mjadala wa jopo kuhusu wanawake katika uongozi uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa rasilimali watu na uongozi kutoka taasisi tofauti, ambapo ilisisitizwa kuwa kuchanganya uzoefu wa vizazi tofauti vya wanawake kazini huleta matokeo chanya pamoja na umuhimu wa kujifunza ujuzi mpya na kuimarisha mentorship baada ya mafunzo.

Washiriki wa kundi la 12 walihimizwa kujenga mitandao imara ya kitaaluma, huku taasisi na makampuni yakitakiwa kutambua upekee wa kila mwanamke badala ya kuwaona kama kundi moja.

Akihitimisha, Mjumbe wa Bodi ya ATE, Bw. Gasper Kikui amesema sekta isiyo rasmi bado ina changamoto nyingi za uongozi na kuwataka washiriki kuyachukulia mafunzo hayo kwa uzito ili kuleta mabadiliko chanya.

Continue Reading

News

Dkt Samia: Vijana wanufaike na uwekezaji katika mawasiliano

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ametaka vijana wanufaike ipasavyo na huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano, hasa katika maeneo ya kukuza ubunifu, ujuzi wa kidigitali na fursa za ajira.

Ametaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, zishirikiane na wadau wa sekta ya teknolojia ili vijana wapate manufaa hayo.

Dkt Samia ameyasema hayo leo, Ijumaa Aprili 10, 2026 jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi huo, ukiambatana na kuunganisha huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 85.

“Uwekezaji huu kwa vijana ni muhimu kwa sababu dunia ya teknolojia ni ya kwao. Dunia hii ipo viganjani mwao na ndiyo mfumo wa maisha yao. Ni lazima tuwawezeshe na kuwahamasisha kutumia mifumo hii ili waweze kukua kiuchumi na kijamii,” amesema.

Continue Reading

News

Dkt Samia azindua minara 758, kuwanufaisha zaidi ya wananchi milioni nane

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Zaidi ya wananchi milioni 8.5 hususan wanaoishi mipakani na vijijini, wanatarajiwa kuondolewa changamoto ya mtandao, baada ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuzindua minara 758 ya mawasiliano iliyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Ijumaa Aprili 10, 2026 jijini Dodoma, ukiambatana na kuunganisha huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 85, ikiwa ni juhudi za Serikali kuimarisha uchumi wa kidijitali na kuongeza huduma za mawasiliano.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt Samia amesema uwekezaji huo umetokana na ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya mawasiliano ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi kwa ubora unaokidhi mahitaji ya teknolojia ya kisasa na kwa gharama nafuu.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa minara hiyo kutachochea ushiriki wa wananchi katika uchumi wa kidijitali na kufungua fursa mpya za ajira, kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo ya Taifa.

“Mawasiliano si tena huduma ya anasa kama ilivyokuwa zamani. Leo hii ni uti wa mgongo wa uchumi wa kisasa na daraja la fursa kwa wananchi katika nyanja mbalimbali za maendeleo,” amesema

Continue Reading

Trending

Copyright © 2025 Newsinfo.