Connect with us

News

Mkutano wa Kilimo Ikolojia hai sasa ni machi 2026

Published

on

Na Mwandishi wetu, News info Online

Shirika la Kilimo Hai Tanzania (TOAM), kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, limetangaza kuahirishwa kwa Mkutano wa Nne wa Kitaifa wa Kilimo Ikolojia Hai (IV NEOAC) ambao sasa utafanyika kuanzia Machi 03 hadi 05, 2026 katika Jiji la Dodoma.

Awali mkutano huo ulipangwa kufanyika Januari 27 hadi 29, 2026, lakini umeahirishwa ili kuimarisha maandalizi na kuruhusu ushiriki mpana wa wadau muhimu.

Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TOAM, Bw. Bakari Mongo, alisema uamuzi wa kuahirisha mkutano umezingatia ubora na tija ya tukio hilo.

“Tunashukuru kwa uvumilivu na uelewa wa wadau wetu. Tarehe hizi mpya zinatupa fursa ya kuandaa mkutano ulio bora zaidi, wenye programu iliyoimarishwa itakayonufaisha Kilimo Ikolojia Hai nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema Mongo.

“Toam radhi wadau wote kwa usumbufu wowote uliotokana na mabadiliko ya tarehe, na imewahakikishia kuwa maandalizi yanaendelea ili kuhakikisha mkutano unakuwa na matokeo chanya na ya kudumu. Taarifa zaidi kuhusu programu iliyosasishwa, wasemaji na usajili zinapatikana kupitia tovuti rasmi ya mkutano.”

Mkutano wa IV NEOAC unatarajiwa kuwakutanisha wadau takribani 400 wakiwemo wakulima, watunga sera, watafiti, wasomi, sekta binafsi, vyama vya kiraia, wabia wa maendeleo pamoja na wanahabari. Washiriki watapata fursa ya kubadilishana maarifa na uzoefu kwa lengo la kuimarisha mifumo endelevu ya uzalishaji wa chakula, kulinda mazingira na kuongeza kipato cha wakulima wadogo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi wa Mtandao wa Mwamvuli wa Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Mwatima Juma, alisema mkutano huo ni jukwaa muhimu kwa mustakabali wa kilimo endelevu nchini.

“IV NEOAC ni fursa adhimu ya kitaifa ya kuimarisha mijadala ya sera, teknolojia na mifumo ya uzalishaji wa chakula endelevu, huku tukikabiliana kwa pamoja na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na usalama wa chakula,” alisema Mwatima Juma.

Maudhui makuu ya mkutano huo ni “Kilimo Ikolojia Hai kwa Mifumo Endelevu ya Chakula”, ambapo majadiliano yataangazia usalama wa chakula na lishe, mbinu na teknolojia za Kilimo Ikolojia Hai, ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, manufaa ya kiuchumi kwa wakulima pamoja na mazingira ya kisera katika kuendeleza sekta hiyo.

Naye Gladness Martin, Mwakilishi wa SWISSAID Tanzania na mdhamini wa mkutano huo, alisema kuwa wameungana kwa pamoja na kukubaliana kuwa kuhairishwa kwa mkutano huo ni mpango wa kuandaa tukio hilo kwa ukubwa zaidi.

Aliongeza kuwa, kutokana na umuhimu mkubwa wa mkutano huo, wameona ni vyema kuchangia jitihada za kuutangaza ndani na nje ya nchi, hususan katika kuibua na kujadili masuala ya kilimo.

Aidha, alisema wanatambua na kuthamini juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuendeleza sekta ya kilimo na kuimarisha mazingira ya mijadala ya maendeleo.

Charles Bupamba, Mwanachama wa Taasisi ya TOAM, aliwaomba wadau kuongeza bidii katika kufuatilia na kuelewa kwa kina masuala ya kilimo hai, pamoja na kushiriki katika kongamano hilo ili kupata fursa ya kujifunza kwa undani elimu ya kilimo na kueneza maarifa yote yanayohusiana na sekta ya kilimo.

Continue Reading
Click to comment
0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

News

Wanawake 142 waanza mafunzo ya Female Future Programme Dar es Salaam

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Zaidi ya wanawake 142 wamepokelewa rasmi kushiriki toleo la 12 la programu ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake, Female Future Programme (FFP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ya kiutendaji yameandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI).

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran amesema programu hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwa zaidi ya wanawake 800 waliokwisha pata mafunzo kwa zaidi ya muongo mmoja, na sasa inaendeshwa katika nchi sita kwa ufadhili wa NHO, huku akiwahamasisha washiriki kushiriki kikamilifu safari ya miezi tisa ya mafunzo. Aidha, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI, Dkt. David Kalaba amesema jamii inahitaji wanawake viongozi wenye kujiamini na uwezo mkubwa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya haraka, akisisitiza umuhimu wa mtazamo wa kimataifa, kujifunza na kuendana na mabadiliko pamoja na uwezo wa kusimamia utofauti, kutatua migogoro na kutoa thamani kwa wateja.

Kwa upande wake, Meneja wa Upstream wa IFC, Bw. Sam Nganga aliyemwakilisha Meneja wa Nchi, Bi. Martine Valcin amesema taasisi hiyo inaendelea kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi katika ngazi za juu za uongozi ili kukuza ushirikishwaji, huku akiwahimiza washiriki kujisimamia na kutumia kikamilifu mafunzo hayo.

Katika hafla hiyo pia kulikuwa na mjadala wa jopo kuhusu wanawake katika uongozi uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa rasilimali watu na uongozi kutoka taasisi tofauti, ambapo ilisisitizwa kuwa kuchanganya uzoefu wa vizazi tofauti vya wanawake kazini huleta matokeo chanya pamoja na umuhimu wa kujifunza ujuzi mpya na kuimarisha mentorship baada ya mafunzo.

Washiriki wa kundi la 12 walihimizwa kujenga mitandao imara ya kitaaluma, huku taasisi na makampuni yakitakiwa kutambua upekee wa kila mwanamke badala ya kuwaona kama kundi moja.

Akihitimisha, Mjumbe wa Bodi ya ATE, Bw. Gasper Kikui amesema sekta isiyo rasmi bado ina changamoto nyingi za uongozi na kuwataka washiriki kuyachukulia mafunzo hayo kwa uzito ili kuleta mabadiliko chanya.

Continue Reading

News

Dkt Samia: Vijana wanufaike na uwekezaji katika mawasiliano

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ametaka vijana wanufaike ipasavyo na huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano, hasa katika maeneo ya kukuza ubunifu, ujuzi wa kidigitali na fursa za ajira.

Ametaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, zishirikiane na wadau wa sekta ya teknolojia ili vijana wapate manufaa hayo.

Dkt Samia ameyasema hayo leo, Ijumaa Aprili 10, 2026 jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi huo, ukiambatana na kuunganisha huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 85.

“Uwekezaji huu kwa vijana ni muhimu kwa sababu dunia ya teknolojia ni ya kwao. Dunia hii ipo viganjani mwao na ndiyo mfumo wa maisha yao. Ni lazima tuwawezeshe na kuwahamasisha kutumia mifumo hii ili waweze kukua kiuchumi na kijamii,” amesema.

Continue Reading

News

Dkt Samia azindua minara 758, kuwanufaisha zaidi ya wananchi milioni nane

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Zaidi ya wananchi milioni 8.5 hususan wanaoishi mipakani na vijijini, wanatarajiwa kuondolewa changamoto ya mtandao, baada ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuzindua minara 758 ya mawasiliano iliyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Ijumaa Aprili 10, 2026 jijini Dodoma, ukiambatana na kuunganisha huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 85, ikiwa ni juhudi za Serikali kuimarisha uchumi wa kidijitali na kuongeza huduma za mawasiliano.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt Samia amesema uwekezaji huo umetokana na ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya mawasiliano ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi kwa ubora unaokidhi mahitaji ya teknolojia ya kisasa na kwa gharama nafuu.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa minara hiyo kutachochea ushiriki wa wananchi katika uchumi wa kidijitali na kufungua fursa mpya za ajira, kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo ya Taifa.

“Mawasiliano si tena huduma ya anasa kama ilivyokuwa zamani. Leo hii ni uti wa mgongo wa uchumi wa kisasa na daraja la fursa kwa wananchi katika nyanja mbalimbali za maendeleo,” amesema

Continue Reading

Trending

Copyright © 2025 Newsinfo.