Connect with us

Uncategorized

NMB Foundation yawanoa Wakulima wa Zao la Kakao Kyela, Serikali yaipongeza

Published

on

NA MWANDISHI WETU, KYELA

SERIKALI imeipongeza Taasisi za NMB Foundation kwa kuendesha Mafunzo kwa Wakulima wa Zao la Kakao kutoka Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) wilayani Kyela, mkoani Mbeya, na kwamba kilichofanywa na taasisi hiyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan.

Mafunzo hayo yaliyolenga Kuongeza Thamani ya Zao la Kakao, Masoko na Uandaaji wa Mpango Biashara, yamefanyika kwa siku nne, yakihusisha washiriki 74 (kutoka AMCOS 37), na kufungwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Bi. Josephine Manase, ambaye alikabidhi vyeti kwa washiriki hao.

Akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo, DC Manase aliipongeza NMB Foundation na Rabo Foundantion kwa kushirikiana na Chama Kikuu cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Kyela (KYECU), kufanikisha mafunzo hayo kwa wadau wa mnyororo wa thamani wa zao la Kakao, kusapoti jitihada za Serikali.

“Ninaposimama hapa kufunga mafunzo haya, basi nianze kwa kuipongeza NMB Foundation na washirika wao Rabo Foundation kwa mafunzo haya, ambayo yanaakisi dhamira yenu ya dhati ya kuliongezea thamani zao la Kakao wilayani Kyela na kukuza uchumi wa wakulima na wadau wake wote.

“Katika hotuba zake nyingi, Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akipongeza ubora wa Kakao ya Kyela, na hiki mlichofanya NMB Foundation, kinaenda kusapoti jitihada za Serikali Kuu na Serikali ya Wilaya ya Kyela katika kuongeza thamani ya zao hili, ambalo limekuwa na mchango mkubwa kiuchumi kwa taifa.

“Wito wangu kwa NMB Foundation na Washiriki, mafunzo haya yasiishie tu darasani, yakaakisi kile mlichojifunza kwa mamia na maelefu ya wanachama wa AMCOS mliowawakilisha, ili kufanikisha mada zilizotolewa hapa ikiwamo ya uchakataji wa Kakao na kuharakisha ukuaji kiuchumi,” alisema Manase.

Alibainisha ya kwamba – iwapo yatatumika vema, basi mafunzo hayo ni nyenzo muhimu katika kubadilisha maisha na uukuaji kiuchumi wa wakulima wilayani mwake, hasa ikizingatiwa aina ya mada zilizotolewa na wakufunzi kutoka NMB Foundation na Rabo Foundation.

“Kupitia mafunzo haya mmejifunza namna ya kuboresha zao la kakao ili kulipa soko la uhakika, kuongeza mapato kupitia uuzaji wa kakao iliyoboreshwa, kufungua fursa za ajira kwa vijana na wanawake walio kwenye mnyororo wa thamani wa zao hili na kupata elimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Zaidi ya hayo, kupitia jukwaa hili wakulima wamepata elimu ya fedha na kujua namna ya kupata mikopo nafuu na kunyanyua kilimo chao, namna usahihi ya matumizi ya mikopo hiyo kwa kunua mahitaji ya msingi ya zao husika na kukuza uzalishaji. Juhudi hizi za NMB Foundation zinapaswa kuigwa na kuendelezwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mratibu wa NMB Foundation Kanda ya Nyanda za Juu, Rodgers Shipella, taasisi yake kwa kushirikiana na Rabo Foundation, wamebuni na kutekeleza mradi wa kuongeza thamani (semi-processing) ya zao la kakao kwa kujenga uwezo wa wakulima kupitia ushirika katika maeneo mbalimbali.

Shipella aliyataja maeneo hayo kuwa ni: “Elimu ya Ushirika, Uongozi Bora Ndani ya Ushirika, Ujasiriamali, Elimu ya Fedha na Usimamizivna Uendeshaji wa Mikopo, Kuongeza Thamani ya Zao, Uhakika wa Masoko ili Kuongeza Uzalishaji na Uchakataji wa Kakao Wilaya ya Kyela.

“NMB Foundation ilianza rasmi utekelezaji wa mradi huu Oktoba 2023 na tangu wakati huo hadi sasa tumefanikiwa kuwafikia wakulima 1,281, wakiwemo wanawake 314 na wanaume 967. Lengo kuu la mradi huu sio tu kuongeza thamani ya zao la kakao, bali pia kuweka uwiano sahihi wa bei.

“Pia mradi huu unalemga kuibua ajira za uchakataji wa kakao kwa vijana na wanawake, ili kutanua njia za makundi hayo kujiongezea kipato cha kila siku na mantiki hiyo, mradi huu sio tu utawanufaisha wakulima na vyama vyao, bali pia wadau wengine kama vile ushirika, Serikali na wanunuzi,” alisema Shipella.

Akifafanua, Shipela alisema wakati Mkulima atapata bei bora na yenye uwiano, uhakika wa soko, kuamsha ari na hamasa ya uboreshaji wa kakao na kuongeza kipato, Serikali za Mitaa na Serikali Kuu nazo zitanufaika kwa kuongeza kipato, kukuza na kuendeleza uzalishaji zao, Kodi ya Thamani (VAT) na PAY E na ajira kwa vijanana wanawake.

Kaimu Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Kyela (KYECU Ltd), Nabii Emmanuel Mwakyenda, aliishukuru NMB Foundation kwa kuwapiga msasa wanachama wa AMCOS 37 za wilaya yake, akiamini mafunzo na elimu waliyopata itakuwa chachu ya ustawi na uendelevu wa Kakao wilayani humo.

Akisoma risala kwa niaba ya washiriki, Evance Mwaipopo kutoka Mwabusye AMCOS, aliipongeza NMB Foundation kwa uendeshaji wa mafunzo, ambayo yamewamenufaisha kupitia mada mbalimbali zikiwamo za Uongezaji Thamani wa Kakao, Kilimo cha Kakao Bila Kukata Miti na Ujasiriamali na Mpango Biashara.

Washiriki wakaiomba NMB Foundation kuendelea kuwajali na kuwathamini wakulima wa kakao Kyela, huku wakiitaka Serikali kwa upande wake izitupie macho barabara zinazoingia na kutoka Kyela, ambazo ni chakavu, ili kurahisisha usafirishaji wa mazao mbalimbali, ikiwemo kakao.

Mwisho

Continue Reading
Click to comment
0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

Uncategorized

NMB Yaandika Historia kwa Kushinda Tuzo Sita Kubwa, Ikiwemo ya “Benki Bora kwa Uendelevu Barani Afrika”

Published

on

By

Dar es Salaam

Benki ya NMB inatangaza mafanikio ya kihistoria ya ushindi wa tuzo sita za kimataifa kutoka kwa majarida mawili mashuhuri duniani – jarida la Euromoney linalochapishwa London, Uingereza, na Global Banking & Finance Magazine lenye makao makuu yake New Jersey, Marekani.

Ushindi huu mkubwa unaashiria kutambuliwa kwa ubora wa huduma, ubunifu na mchango wa Benki ya NMB katika kuchangia maendeleo endelevu ya kiuchumi nchini.

Miongoni mwa tuzo hizo ni ile ya heshima ya “Benki Bora kwa Uendelevu Barani Afrika” inayodhibitisha mafanikio na maendeleo makubwa ya NMB na tasnia nzima ya fedha nchini.

Tuzo ya “Benki Bora kwa Uendelevu Barani Afrika”, iliyotolewa hivi karibuni jijini London katika hafla ya Euromoney Private Banking Awards 2025, imeweka historia kwa kuwa ya kwanza kutolewa kwa Benki ya Kitanzania.. Hii ni hatua kubwa ya kutambua mchango wa Tanzania katika eneo nyeti la uendelevu, ambalo lina umuhimu mkubwa katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na mazingira duniani kote.

Ushindi huu unadhihirisha jitihada za Benki ya NMB za kuongoza mabadiliko na dhamira yake ya dhati za kuyafanya masuala ya mazingira, jamii na utawala bora (ESG) kuwa sehemu ya msingi katika shughuli zake za kiutendaji na dira yake ya kimkakati.

Benki ya NMB pia ilinyakua tuzo mbalimbali kama kinara wa kitaifa katika sekta ya benki kutoka kwa majarida hayo mawili kama ifuatavyo:

Euromoney:
● Benki Bora ya Uendelevu Tanzania
● Benki Bora ya Wateja Maalum Tanzania (kwa mwaka wa tatu mfululizo)

Global Banking and Finance Magazine:
● Benki Salama Zaidi Nchini Tanzania
● Kinara wa Uwajibikaji kwa Jamii Tanzania 2025
● Afisa Mtendaji Mkuu Bora wa Benki Tanzania 2025 (Tuzo hii ilitolewa kwa CEO Ruth Zaipuna)

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi Ruth Zaipuna alipongeza kwa tuzo hizo huku akisema : “Ni hatua ya kihistoria kwa tasnia ya fedha nchini. Aidha, alisisitiza kuwa tuzo hizi ni hatua muhimu katika kuisaidia Tanzania kujipambanua kama kiongozi wa kikanda wa ufadhili endelevu na utoaji wa huduma bora za kifedha.

“Ni heshima kubwa kwetu kutambuliwa na Euromoney na Global Banking & Finance Magazine kwa uongozi wetu katika Ufadhili Endelevu na Huduma kwa Wateja Maalum,” alisema Bi. Zaipuna. “Tuzo hizi sita ni ushahidi wa juhudi na kujitolea kwa wafanyakazi wetu,, imani kubwa ambayo wateja wetu wameendelea kutuonesha, na dhamira thabiti tuliyonayo ya kujenga mustakabali wa ustawi, ujumuishaji, na maendeleo endelevu kwa nchi yetu.”

“Sisi kama Benki ya NMB, uendelevu si tu ni wajibu wa kibiashara bali ni hitaji la kimkakati linalochangia uimara wa biashara, kuchochea ubunifu, kuongeza ushindani, na kuhakikisha upatikanaji wa thamani ya kudumu. Kwa kuufanya uendelevu kuwa kiini cha mkakati wetu wa biashara, tunawahakikishia wadau wetu thamani ya kudumu na kuwa na athari chanya kwa jamii tunazozihudumia.”

Benki ya NMB pia imepata heshima ya kutambuliwa kama Benki Salama Zaidi nchini Tanzania kutokana na dhamira yake thabiti katika maendeleo ya kiteknolojia na rasilimali watu.

“Tuzo hii ni matokeo ya moja kwa moja ya uwekezaji wa kimkakati katika ubunifu na hatua madhubuti za usalama wa mtandao, hali inayowezesha uwepo wa mazingira ambayo yanafanya wateja zaidi ya milioni 8.6 kuwa na imani na uimara wa kifedha wa Benki ya NMB na usalama wa fedha zao.

“Tumejidhatiti kukuza uwezo wetu na kuhakikisha ufanisi wa kifedha wa kudumu, tutaendelea kuwekeza katika teknolojia na rasilimali watu ili kukidhi mahitaji anuwai ya wateja wetu tunaowathamini kwa moyo wote,” alihitimisha Bi. Zaipuna.

Akizungumzia tuzo hizo, Mhariri Mkuu wa Euromoney, Bi. Louise Bowman, alisema, “Benki ya NMB imedhihirisha kuwa taasisi kinara wa maendeleo endelevu nchini Tanzania na barani Afrika kupitia mipango yake ya kimkakati inayozingatia uwiano wa uwajibikaji wa kimazingira, athari chanya kwa jamii, na ukuaji wa kifedha.”

Tuzo hizi zinabainisha dhamira ya Benki ya NMB katika uendelevu wa mazingira na jamii, sambamba na kutoa masuluhisho bora ya kifedha yenye viwango vya kimataifa, ambayo yanawawezesha wateja na kuchochea maendeleo jumuishi ya kiuchumi. Kutambuliwa huku ni uthibitisho wa maono ya kimkakati ya Benki ya NMB katika kuendeleza Ukuaji Jumuishi na Maendeleo Endelevu, huku ilipanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania wote.

Benki ya NMB inaendeleza kwa dhati dhamira yake ya kuzingatia viwango vya juu kabisa vya ubora wa huduma za kibenki, kuendeleza ubunifu, na kuchangia kikamilifu katika maendeleo endelevu ya Tanzania chini ya uongozi wa ushindi wa Bi. Zaipuna.

Continue Reading

Trending

Copyright © 2025 Newsinfo.