Connect with us

News

Kamishna wa Bima atoa wito kwa vyombo vya habari kufichua udanganyifu sekta ya bima

Published

on

Na Mwandishi wetu, Newsinfo Online

Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo Saqware, ametoa wito kwa wahariri na vyombo vya habari kufuatilia kwa karibu kesi za udanganyifu wa bima zinazoendelea katika mahakama mbalimbali nchini, ili kusaidia kuilinda sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa taifa.

Akizungumza jana katika mafunzo ya wahariri wa habari kuhusu masuala ya bima na umuhimu wa Taarifa ya Soko la Bima, Dkt. Saqware alisema ushirikiano kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na vyombo vya habari ni muhimu katika kuhakikisha sekta hiyo inakuwa kichocheo cha maendeleo ya uchumi wa nchi.

“Vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kufichua wadanganyifu wa bima. TIRA ipo tayari kushirikiana nanyi katika kukuza uelewa na kutoa mafunzo mnapohitaji,” alisema.

Aidha, aliwataka wahariri kuongeza weledi katika uandishi wa masuala ya bima na kutoa kipaumbele kwa habari zinazohusu sekta hiyo kwani zinagusa maisha ya wananchi wote kutoka kwa wafanyabiashara wadogo hadi wawekezaji wakubwa.

Dkt. Saqware pia aliwahimiza wahariri kuendelea kutumia Taarifa ya Soko la Bima kama nyenzo muhimu ya uchambuzi wa habari, akisema taarifa hizo ni msingi wa uandishi wenye tija na unaozingatia takwimu sahihi.

Akizungumzia mwenendo wa sekta hiyo, Kamishna huyo alisema bima nchini imekuwa ikionyesha ukuaji mzuri mwaka hadi mwaka sambamba na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia.

Kwa mujibu wa takwimu za karibuni, ongezeko la matumizi ya teknolojia, maboresho ya mifumo ya usajili na usimamizi wa kampuni za bima pamoja na kuimarisha udhibiti kumeongeza uaminifu na ushindani katika soko.

Kwa sasa Tanzania ina zaidi ya kampuni 40 za bima pamoja na mawakala, madalali na watoa huduma wengine wanaotoa bidhaa na huduma mbalimbali kwa wananchi. Hata hivyo, aliweka wazi kuwa bado kuna changamoto ya uelewa mdogo wa wananchi kuhusu umuhimu wa bima, eneo ambalo vyombo vya habari vinaweza kubadilisha kwa kutoa elimu sahihi.

Dkt. Saqware alisema sekta ya bima ina mchango mkubwa katika uchumi, kwani huduma za bima huwezesha uwekezaji, kuimarisha ujasiriamali na kutoa ulinzi kwa wananchi dhidi ya majanga kama moto, ajali, majanga ya asili na magonjwa.

Pia, katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama nishati, reli, barabara na viwanda, bima imeendelea kuwa nguzo muhimu ya kuhakikisha uwekezaji unafanyika bila kuhatarisha maisha ya watu na mali za taifa.

Aliongeza kuwa matumizi ya bima ya kilimo yameendelea kuwasaidia wakulima kupunguza hasara zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi, hali inayochangia katika uhakika wa chakula nchini.

Aidha, aliainisha baadhi ya hatua ambazo TIRA imeendelea kuchukua ili kuifanya sekta ya bima kuwa imara, ya kisasa na yenye manufaa kwa wananchi. Hatua hizo ni pamoja na Kuboresha mifumo ya usimamizi na udhibiti kupitia teknolojia, Kuanzisha na kusimamia mifumo ya kidijitali ya usajili wa bima kama Online Registration System (ORS), Kuimarisha ukaguzi wa kampuni za bima ili kuhakikisha zinatimiza wajibu wao kwa wananchi, Kutoa elimu kwa umma kupitia redio, televisheni, mitandao ya kijamii na mikutano ya wadau na Kushirikiana na taasisi za kimataifa kuboresha uwezo wa sekta ndogo ya bima nchini.

Kwa upande wake Margaret Mngumi – Msuluhishi wa Migogoro ya Bima kutoka Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima Tanzania (TIO) alisema TIO imekuwa kiungo muhimu kati ya wananchi, kampuni za bima na Serikali, na imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utatuzi wa migogoro ya bima hapa nchini.

Aidha alisisitiza kwamba Vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika Kufikisha elimu sahihi kwa wananchi kuhusu hatua za kudai fidia, Kusaidia kupunguza malalamiko yasiyo na msingi kwa kutoa taarifa sahihi, Kuelimisha umma dhidi ya udanganyifu wa madai ya bima (insurance fraud), na Kuimarisha uwajibikaji wa kampuni za bima kupitia uandishi wa uwazi na wa haki.

TIO inatambua nguvu mlizo nazo, na tungependa leo tuanzishe ukurasa mpya wa ushirikiano, ili kuboresha zaidi mazingira ya utatuzi wa migogoro ya bima kwa maslahi ya Watanzania. Na Jackline Martin

TIO inatambua nguvu mlizo nazo, na tungependa leo tuanzishe ukurasa mpya wa ushirikiano, ili kuboresha zaidi mazingira ya utatuzi wa migogoro ya bima kwa maslahi ya Watanzania.

Continue Reading
Click to comment
0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

News

Wanawake 142 waanza mafunzo ya Female Future Programme Dar es Salaam

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Zaidi ya wanawake 142 wamepokelewa rasmi kushiriki toleo la 12 la programu ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake, Female Future Programme (FFP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ya kiutendaji yameandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI).

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran amesema programu hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwa zaidi ya wanawake 800 waliokwisha pata mafunzo kwa zaidi ya muongo mmoja, na sasa inaendeshwa katika nchi sita kwa ufadhili wa NHO, huku akiwahamasisha washiriki kushiriki kikamilifu safari ya miezi tisa ya mafunzo. Aidha, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI, Dkt. David Kalaba amesema jamii inahitaji wanawake viongozi wenye kujiamini na uwezo mkubwa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya haraka, akisisitiza umuhimu wa mtazamo wa kimataifa, kujifunza na kuendana na mabadiliko pamoja na uwezo wa kusimamia utofauti, kutatua migogoro na kutoa thamani kwa wateja.

Kwa upande wake, Meneja wa Upstream wa IFC, Bw. Sam Nganga aliyemwakilisha Meneja wa Nchi, Bi. Martine Valcin amesema taasisi hiyo inaendelea kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi katika ngazi za juu za uongozi ili kukuza ushirikishwaji, huku akiwahimiza washiriki kujisimamia na kutumia kikamilifu mafunzo hayo.

Katika hafla hiyo pia kulikuwa na mjadala wa jopo kuhusu wanawake katika uongozi uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa rasilimali watu na uongozi kutoka taasisi tofauti, ambapo ilisisitizwa kuwa kuchanganya uzoefu wa vizazi tofauti vya wanawake kazini huleta matokeo chanya pamoja na umuhimu wa kujifunza ujuzi mpya na kuimarisha mentorship baada ya mafunzo.

Washiriki wa kundi la 12 walihimizwa kujenga mitandao imara ya kitaaluma, huku taasisi na makampuni yakitakiwa kutambua upekee wa kila mwanamke badala ya kuwaona kama kundi moja.

Akihitimisha, Mjumbe wa Bodi ya ATE, Bw. Gasper Kikui amesema sekta isiyo rasmi bado ina changamoto nyingi za uongozi na kuwataka washiriki kuyachukulia mafunzo hayo kwa uzito ili kuleta mabadiliko chanya.

Continue Reading

News

Dkt Samia: Vijana wanufaike na uwekezaji katika mawasiliano

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ametaka vijana wanufaike ipasavyo na huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano, hasa katika maeneo ya kukuza ubunifu, ujuzi wa kidigitali na fursa za ajira.

Ametaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, zishirikiane na wadau wa sekta ya teknolojia ili vijana wapate manufaa hayo.

Dkt Samia ameyasema hayo leo, Ijumaa Aprili 10, 2026 jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi huo, ukiambatana na kuunganisha huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 85.

“Uwekezaji huu kwa vijana ni muhimu kwa sababu dunia ya teknolojia ni ya kwao. Dunia hii ipo viganjani mwao na ndiyo mfumo wa maisha yao. Ni lazima tuwawezeshe na kuwahamasisha kutumia mifumo hii ili waweze kukua kiuchumi na kijamii,” amesema.

Continue Reading

News

Dkt Samia azindua minara 758, kuwanufaisha zaidi ya wananchi milioni nane

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Zaidi ya wananchi milioni 8.5 hususan wanaoishi mipakani na vijijini, wanatarajiwa kuondolewa changamoto ya mtandao, baada ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuzindua minara 758 ya mawasiliano iliyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Ijumaa Aprili 10, 2026 jijini Dodoma, ukiambatana na kuunganisha huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 85, ikiwa ni juhudi za Serikali kuimarisha uchumi wa kidijitali na kuongeza huduma za mawasiliano.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt Samia amesema uwekezaji huo umetokana na ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya mawasiliano ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi kwa ubora unaokidhi mahitaji ya teknolojia ya kisasa na kwa gharama nafuu.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa minara hiyo kutachochea ushiriki wa wananchi katika uchumi wa kidijitali na kufungua fursa mpya za ajira, kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo ya Taifa.

“Mawasiliano si tena huduma ya anasa kama ilivyokuwa zamani. Leo hii ni uti wa mgongo wa uchumi wa kisasa na daraja la fursa kwa wananchi katika nyanja mbalimbali za maendeleo,” amesema

Continue Reading

Trending

Copyright © 2025 Newsinfo.