Connect with us

News

Maaskofu, Masheikh nyandaza juu wahimiza uchaguzi wa amani

Published

on

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

VIONGOZI wa dini kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, huku wakisisitiza umuhimu wa kudumisha amani kabla, wakati na baada ya Uchaguzi huo.

Viongozi hao kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa wametoa kauli hiyo leo Oktoba 23, 2023 katika Kongamano la Amani na Uchaguzi lililofanyika jijini Mbeya.

Mwishoni mwa kongamano hilo lililoongozwa na kauli mbiu ‘Kupiga kura ni haki yetu na kulinda amani ni wajibu wetu’, viongozi wa Dini wamesoma maazimio, yanayosisitiza ulinzi wa amani ya nchi na kuhimiza wananchi kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akisoma tamko rasmi la viongozi wa dini wa Nyanda za Juu Kusini, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la TAG ICC Mbeya, Askofu Profesa Donald Mwanjoka, amesema moja ya maazimio ni kuwataka wananchi wote waliopata nafasi ya kujiandikisha kujitokeza siku ya uchaguzi, kufanya maamuzi ya busara na kuchagua viongozi waadilifu watakaotumikia kwa uaminifu.

“Tunawakumbusha wananchi wote kwamba kushiriki katika Uchaguzi ni haki ya kikatiba na wajibu wa kizalendo. Amani ni msingi wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiroho, hivyo tofauti za kisiasa hazipaswi kuwa chanzo cha chuki, maandamano au vurugu,” amesema Prof. Mwanjoka, kwa niaba ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) na Kamati za Amani za mikoa hiyo.

Viongozi hao pia walitoa wito kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, haki na wa kuaminika, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikisisitizwa kuzingatia utu, sheria na haki za binadamu wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Sheikh wa Mkoa wa Mbeya na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa huo, Sheikh Msafiri Njalambaha, amesema amani ni msingi wa maisha ya ibada na ustawi wa taifa.

“Hakuna Uchaguzi, maendeleo, wala ibada bila amani. Kura ni haki yetu, amani ni wajibu wetu,” amesema.

Askofu Oscar Ongele ambaye ni Mwenyekiti wa JMAT Mkoa wa Mbeya, amewasihi viongozi wa dini kutumia nyumba za ibada kuhamasisha waumini waliojiandikisha kwenda kupiga kura kwa amani.

“Tujitokeze kwa wingi, tuwahimize waumini wetu washiriki bila hofu, kwa sababu vyombo vya ulinzi na usalama vipo kulinda amani yetu,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Iringa, Dk. Joseph Mgumi, amesema hakuna maendeleo bila uongozi na hakuna uongozi bila Uchaguzi, hivyo ni muhimu kila Mtanzania kushiriki. “Tupige kura kwa wingi ili tupate viongozi watakaotuletea maendeleo,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Songwe, Sheikh Alhaj Batuza, amesisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa kila jambo. “Wazee wetu walihangaika kuupata uhuru. Leo sisi tunapaswa kuilinda amani kwa vitendo, si kwa maneno,” alisema.

Aidha, Askofu Mstaafu Ambele Mwaipopo wa KKKT Dayosisi ya Ziwa Tanganyika (Rukwa) amewakumbusha wananchi kuwa ni wajibu wa kila mmoja kulinda amani aliyopewa na Mungu. “Asicheze mtu na amani ya taifa letu; kila mmoja awe mlinzi wa amani,” amesema.

Sheikh wa Wilaya ya Njombe (mkoani Njombe), Shabani Dinga amewahamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura kwa amani, huku akisisitiza umuhimu wa uvumilivu na ukomavu wa kisiasa.

Naye Askofu Jacob Kahemele wa Kanisa la Anglikana Mbeya amesema tofauti za kisiasa hazipaswi kugawa watu. “Uchaguzi ni mchakato wa kawaida wa kidemokrasia. Tuwe na hekima, tuvumiliane, tushiriki kwa amani,” amesema.

Kwa upande wake, Askofu Erica Mwakyokile wa Kanisa la Pentecost Shilo Mkoa wa Mbeya, amewahamasisha Watanzania kuendelea na maombi katika nyumba za ibada hadi Uchaguzi utakapopita. “Kila mtu yuko hapa kwa sababu ya amani, tuendelee kuomba ili Tanzania iendelee kuwa nchi ya utulivu,” alisema.

Viongozi hao kwa pamoja walihitimisha kwa kuwataka Watanzania kutambua kuwa kura moja inaweza kuandika historia mpya ya taifa, hivyo wajitokeze kupiga kura kwa amani, umoja na uzalendo, wakiweka mbele maslahi ya nchi kuliko ya mtu binafsi.

Continue Reading
Click to comment
0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

News

Wanawake 142 waanza mafunzo ya Female Future Programme Dar es Salaam

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Zaidi ya wanawake 142 wamepokelewa rasmi kushiriki toleo la 12 la programu ya mafunzo ya uongozi kwa wanawake, Female Future Programme (FFP), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ya kiutendaji yameandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Taasisi ya Usimamizi ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI).

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba-Doran amesema programu hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwa zaidi ya wanawake 800 waliokwisha pata mafunzo kwa zaidi ya muongo mmoja, na sasa inaendeshwa katika nchi sita kwa ufadhili wa NHO, huku akiwahamasisha washiriki kushiriki kikamilifu safari ya miezi tisa ya mafunzo. Aidha, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI, Dkt. David Kalaba amesema jamii inahitaji wanawake viongozi wenye kujiamini na uwezo mkubwa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya haraka, akisisitiza umuhimu wa mtazamo wa kimataifa, kujifunza na kuendana na mabadiliko pamoja na uwezo wa kusimamia utofauti, kutatua migogoro na kutoa thamani kwa wateja.

Kwa upande wake, Meneja wa Upstream wa IFC, Bw. Sam Nganga aliyemwakilisha Meneja wa Nchi, Bi. Martine Valcin amesema taasisi hiyo inaendelea kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi katika ngazi za juu za uongozi ili kukuza ushirikishwaji, huku akiwahimiza washiriki kujisimamia na kutumia kikamilifu mafunzo hayo.

Katika hafla hiyo pia kulikuwa na mjadala wa jopo kuhusu wanawake katika uongozi uliowashirikisha wataalamu mbalimbali wa rasilimali watu na uongozi kutoka taasisi tofauti, ambapo ilisisitizwa kuwa kuchanganya uzoefu wa vizazi tofauti vya wanawake kazini huleta matokeo chanya pamoja na umuhimu wa kujifunza ujuzi mpya na kuimarisha mentorship baada ya mafunzo.

Washiriki wa kundi la 12 walihimizwa kujenga mitandao imara ya kitaaluma, huku taasisi na makampuni yakitakiwa kutambua upekee wa kila mwanamke badala ya kuwaona kama kundi moja.

Akihitimisha, Mjumbe wa Bodi ya ATE, Bw. Gasper Kikui amesema sekta isiyo rasmi bado ina changamoto nyingi za uongozi na kuwataka washiriki kuyachukulia mafunzo hayo kwa uzito ili kuleta mabadiliko chanya.

Continue Reading

News

Dkt Samia: Vijana wanufaike na uwekezaji katika mawasiliano

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ametaka vijana wanufaike ipasavyo na huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano, hasa katika maeneo ya kukuza ubunifu, ujuzi wa kidigitali na fursa za ajira.

Ametaka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, zishirikiane na wadau wa sekta ya teknolojia ili vijana wapate manufaa hayo.

Dkt Samia ameyasema hayo leo, Ijumaa Aprili 10, 2026 jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi huo, ukiambatana na kuunganisha huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 85.

“Uwekezaji huu kwa vijana ni muhimu kwa sababu dunia ya teknolojia ni ya kwao. Dunia hii ipo viganjani mwao na ndiyo mfumo wa maisha yao. Ni lazima tuwawezeshe na kuwahamasisha kutumia mifumo hii ili waweze kukua kiuchumi na kijamii,” amesema.

Continue Reading

News

Dkt Samia azindua minara 758, kuwanufaisha zaidi ya wananchi milioni nane

Published

on

By

Na Mwandishi wetu, News info

Zaidi ya wananchi milioni 8.5 hususan wanaoishi mipakani na vijijini, wanatarajiwa kuondolewa changamoto ya mtandao, baada ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuzindua minara 758 ya mawasiliano iliyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Ijumaa Aprili 10, 2026 jijini Dodoma, ukiambatana na kuunganisha huduma za mkongo wa Taifa wa mawasiliano katika Wilaya 85, ikiwa ni juhudi za Serikali kuimarisha uchumi wa kidijitali na kuongeza huduma za mawasiliano.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt Samia amesema uwekezaji huo umetokana na ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya mawasiliano ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi kwa ubora unaokidhi mahitaji ya teknolojia ya kisasa na kwa gharama nafuu.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa minara hiyo kutachochea ushiriki wa wananchi katika uchumi wa kidijitali na kufungua fursa mpya za ajira, kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo ya Taifa.

“Mawasiliano si tena huduma ya anasa kama ilivyokuwa zamani. Leo hii ni uti wa mgongo wa uchumi wa kisasa na daraja la fursa kwa wananchi katika nyanja mbalimbali za maendeleo,” amesema

Continue Reading

Trending

Copyright © 2025 Newsinfo.